Moja kati ya nyimbo zilizofanya vyema ndani ya mwaka huu tena ndani ya muda mfupi ni pamoja na wimbo wa mwanadada Angel Bernard unaokwenda kwa jina la Siteketei. Wimbo huu ambao tayari umeshakuwa wimbo wa taifa nchini Tanzania na duniani kwa ujumla, kwa wiki moja umeweza kufikisha viewers 255,200.huku watu maarufu nchini humo wakionekana kuupenda kiasi cha kuamua kujirekodi na kupost wakiuimba wimbo huo kama alivyofanya muigizaji Elizabeth Michael a.k.a Lulu

Si hivyo tu, mwanadada huyu ambaye kwasasa anatarajia kupata mtoto mwaka huu, anavunja rekodi ya kuwa nominated mare nyingi zaidi katika Tuzo mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwemo Uingereza pamoja na U.S.A.

Mtandao huu utakupa habari zaidi juu ya kazi za mwanamuziki huyu wa muda mrefu, pamoja na stori balimbali za maisha yake.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here