Na; Bomby Johnson

Kuna Changamoto nyingi katika mziki wa Injili hapa kwetu… lakini hakuna kazi isiyo na changamoto popote duniani. Na hakuna huduma iliyosimama bila kupitia majaribu na kuyashinda.
Ugumu wa maisha, mtu yeyote anaweza pitia.
Tambua Nchi au Taasisi yoyote ile inaweza pata mtikisiko wa kiuchumi. Maisha ni kupata ama kukosa. Lakini mwenye bidii hufanikiwa.
Tuweni makini sana na mbinu ama njia tunazotumia kujikwamua kiuchumi. Kuna njia zingine ni mitego ya ibilisi katika kuua huduma au maisha ya mtu. Maana hata shetani anajua nini unataka au unachotafuta. Na yeye pia anaweza akakupa ofa na ukapata utakacho lakini kitakacho kumaliza hapo baadae.
Wewe kamwe usiruhusu hayo.


Siku hizi kuna elimu nyingi na hata waelimishaji wanashindana kuelimisha.
Asije akakudanya mtu na kukwaminisha kwamba unaweza kila kitu kwa kutumia akili na nguvu binafsi pekee… hiyo haitoshi.
unamuhitaji Mungu na unawahitaji watu wa kukusaidia maishani.
Hivyo nidhamu binafsi na hekima iliyo ndani
Yako ikusaidie kuchagua nini au nani anakufaa na nani hakufai.

Alafu kumbuka Mungu ni Mungu wa maagano
Je unalikumbuka agano lako na Mungu?
Usiyumbishwe, simama katika Imani.
Si kila makofi ni ya kuungwa mkono
Mengine ni ya kufurahia unavyoanguka
Kama vile Mungu asivyolala halikadhalika
Shetani naye halali.
Shinda hali hiyo, Shinda vita hiyo.
Maana mkono wa Bwana u pamoja nawe!

Hii inahusu mtumishi aliyeitwa…
Mungu akubariki sana.

By Pastor B.Johnson

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here